Alhamisi, 4 Oktoba 2018

Lengo la mashetan

بسم الله الرحمن الحيم.

NINI LENGO LA MASHETANI KUMUAMRISHA MJA KUFANYA IBADA?

Utawasikia wanasema.

Alhamdulillaahi Mashetani yake yanampeleka kwenye kheri.

(a)Wamemuamrisha kuswali mpaka sasa hivi anaswali.

(b) Akizini wanapanda na kukemea hawataki uchafu na tena ataumwa.

(c) Hawataki atembee kichwa wazi bila ya kujifunika, sasa hivi ushungi na mtu.

(d) Wanamlinda kila wakimwendea wachawi anapandisha na kuwakimbiza.

(e) Hawataki anywe pombe akinywa anaumwa kwelikweli.

(f) Asikubali kuolewa hao ndiyo watakao mchagulia mume bora.

(g) Watamfundisha uganga ili asaidie watu maana jamii inateseka kwa maradhi na shida mbalimbali.

(h) Kuamrisha kilinge kifungwe mwezi wa Ramadhani kwa sababu ni mwezi mtukufu haifai kucheza ngoma, ni mwezi wa toba .

(i) Akiolewa ni lazima ashikwe sikio tujulishwe, akipata mimba tujulishwe, akizaa tujulishwe, ili tumlinde na ubaya wa mahasidi.

Maneno hayo ukiyatazama ni mazuri, lakini lengo ni baya kwa mwenye kuyakubali.

Aliwahi kusema Aliy bnu Abiy Twaalibi Allah amridhie.

.كلمـــــــة حق أريد بهــــــا باطل.

Maneno ya kweli lakini lengo ni batili.

lkiwa Allah na Mtume wake wamekuamrisha kufanya mema na kuacha mabaya huku wakikuonya endapo utapuuza basi utaadhibiwa, na Allah ni mkali wa kuadhibu kuliko yeyote yule.

Yawaje Allah umpuuze halafu ufanye utiifu kwa kumuogopa  Shetani ambae hana uwezo wa kukuadhibu kumshinda Allah mtukufu?, huo ni ujinga.

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ.

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi (Alkawthar - 2).

Ina maana yote hayo uliyo mkabidhi Shetani huamini kwamba Mola wako anaweza kuyasimamia?, Au wewe ni katika wale alio wataja Allah katika aya hii tukufu?.

اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّهِ ۚ أُولَٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ.

Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi la Shetani ndilo lenye kupata khasara (Mujaadilah 19).

Kama ulikua hujui leo jua kwamba Allah ndiye mlinzi pekee kwako, hao Mashetani unao wategemea ni kujidanganya tu na kujipeleka Jahannamu.

اللَّهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُمْ مِنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ.

Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu(Albaqarah - 257).

Hivi mpaka leo hujaelewa na kuzingatia mafundisho haya ya Mtume wako swalla llaahu alayhi wasallama pindi alipokua akimfundisha Swahaba wake lbnu Abbaasi Allah amridhie yeye na baba yake?.

إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللَّهِ وَاعْلَمْ أَنَّ الْأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ لَكَ وَلَوْ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إِلَّا بِشَيْءٍٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ.ُ(رواه الترمذي عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ).

Ukitaka kuomba muombe Allah, na  ukitaka msaada taka msaada kwa Allah, Tambua hakika watu lau walijikusanya ili kukunufaisha, hawato kunufaisha ila kwa lile alilo kuandikia Allah, Na lau watu wakijikusanya ili kukudhuru hawato kudhuru ila lile alilo kuandikia Allah (Ameipokea Tirmidh kutokana na lbnu Abbaas).

Huo uganga hautokosa kupiga Ramli na kuwapa wagonjwa masharti yaambatanayo na Shirki kama kumchinjia jini n.k.

  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ
  ،من أتى عرافاً فسأله عن شيء فصدقه لم تقبل له صلاة أربعين يوما ( ، رواه مسلم)

Amesema Mtume swalla llaahu alayhi wasallama, Mwenye kumuendea  mpiga Ramli akamuuliza jambo na akamsadiki basi haikubaliwi swala kwake siku arobaini ( Muslimu).

  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ : مَنْ أَتَى عَرَّافًا أَوْ كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ فِيمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ (رواه الحاكم).

Amesema Mtume swalla llaahu alayhi waalihi wasallama, Mwenye kumwendea Mpiga ramli au Kuhani na akamsadikisha katika ayasemayo, Hakika amekufuru kilicho teremka kwa Muhamadi (Alhaakimu)

Shetani ni Shetani hawezi kuwa mwema hata siku moja atabaki kuwa adui, hizo ni ghiliba za kuwafanya watu wajinga  wamtii kwa sababu ya maslahi madogo ya duniani  ili aende nao motoni.

إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ

Hakika Shet'ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni (Alfaatwir-6).

kama una Mashetani wa tabia hiyo usijidhanie umepata bado huo ni upotevu,  kasomewe Ruqya uondokane na  ibada za kuwatii Mashetani.

Sisi kazi yetu ni kubainisha, mwenye kuongoa ni Allah pekee.big
.0715849684