Ijumaa, 14 Desemba 2018

Kijicho na sababu zake

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.

SABABU ZA KUPATWA NA UCHAWI,JINI,HASADI NA KIJICHO.

Amesema Allah aliyetukuka.

له معقبا ت من بين يديه ومن خلفه يحفظونه من أمر الله

Kila mtu analo kunda la Malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu(Arraad 11).

Allah mtukufu ametuahidi ulinzi kutokana na mambo mbalimbali,wapo wapatwao na matatizo kama mitihani tu Allah amewakadiria ili kuwapima imani zao na halina kuhoji hilo.

لا يسئل عما يفعل وهم يسأ لون.

Haulizwi (Allah) afanyalo bali hao (waja) ni wenye kuulizwa.(Al -anbiyaai 23)

Wengine hupatwa na mitihani kwa njia ya kuwaonya kutokana na makosa yao ili wamrejee Mola wao.

وما أصابكم من مصيبة فبما كسبت أيديكم.

Na haiwi kwa yanayo kupateni kutokana na majanga ni yale yaliyo tokana na mikono yenu.(Ashuuraa 30).

Tutakuletea sababu miongoni mwa sababu za mja kupatwa na mitihani ya Uchawi,Kijicho,Hasadi na Mashetani wa kijini.

(1)Kujiweka mbali na Allah mtukufu,kwani mwenye kuwa mbali na Mola wake rafiki yake ni shetani na ataishi maisha ya dhiki,na mwenye kuwa karibu na Allah basi huhifadhiwa.

(2)Kufanya sherehe zenye munkari na haramu ndani yake na upuuzi, kama Rusha roho,matarumbeta, vigodoro n.k,kwani shetani hushiriki katika sherehe hizo na huwa rahisi kumpata amtakae kwa kumuingia na kumuwekea uchawi.

(3) Kuogopa sana Uchawi mpaka hofu ya Allah ikamuondoka mtu, ikawa haamini kama Allah anaweza kumuhifadhi na shari za wachawi.

(4) Kutosoma Adhkari za asubuhi na jioni pamoja na kupuuza adhkari za kulalia pamoja na adhkari nyinginezo kama kuingia chooni n.k.

(5)Mwanadamu kumtamani jini kama kumuoa au kuolewa na jini,au jini kumtamani mwanadamu kimapenzi na ikawa mtu huyo hafanyi adhkari yoyote.

(6)Mwanadamu kumuudhi jini kwa kumrushia kitu kama takataka,kummwagia maji ,kumkwaa au kumkanyaga na ikawa mtu huyo hana Adhkari,jini hughadhibika na kumuingia kwa urahisi.

(7) Kulala uchi au na nguo zenye kuonesha umbile la mtu na ikawa amelala bila ya kusoma Adhkari za kulalia.

(8)Kupenda tabia za kishetani kama kuigiza katika Filam mtu yeye ni jini au Zimwi.

(9)Kutembea ufukweni mwa bahari na kuogelea na pia kukaa maeneo hayo na viguo vifupi hali ya kuwa hajasoma adhkari za kinga mtu huyo asubuhi na jioni.

(10)Kukaa chooni muda mrefu iwe kujisaidi au kupenda tu kuchezea maji huko chooni.

(11) Kupenda kuzungumza au kuimba au kulia akiwa chooni.

(12) Kutotajwa Mwenyezi Mungu ndani ya nyumba kwa kutosomwa Qurani au kusikilizwa mawaidha,ikawa ni nyumba ya muziki na  Tamthilia.

(13)Kufaya madhambi makubwa kama Uzinifu,Ulawiti,Ulevi,Wizi,Ushirikina na mengine mfano wa hayo.

(14)Kuhuzunika sana baada ya tukio la simanzi hadi kuchanganyikiwa,kama kufiwa au kufurahi sana kupita kiasi hadi kukufuru kama kuvua nguo mbele za watu,kucheza ngoma na kadhalika.

(15)Kurusha mawe sehemu zilizo hamwa kama magofu,magari mabovu,mapango na miti mikubwa.

Hayo yote endapo yatafanywa na mtu asiyesoma adhkari za kujikiga asubuhi na jioni basi ni rahisi kupatikana na majini,uchawi ,hasadi na kijicho.

Tubadilikeni ndiyo ufumbuzi wa matatizo yetu.

إن الله لا يغير ما بقوم حتى يغير ما بأنفسهم

Hakika Allah habadilishi yaliyo kwa watu mpaka wabadilishe yaliyoko nafsini mwao.(Arraad 11).

Kwa tiba nasaha na ushauri wasiliana nami +255715849684

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni