Jumatano, 18 Mei 2016

Jitibu vidonda

KUTIBU VIDONDA KWA KUTUMIA ASALI

ASALI ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu vidonda na ambayo imekua ikitumika kwa miaka mingi sana. Historia inaonyesha hata wakati wa vita zamani wanajeshi walikua wanatumia Asali kutibu vidonda!!

Kwanini Asali inatibu vidonda???

Asali ina tabia na faida zifuatazo ambazo zinasaidia uponyeshaji hasa hasa ukitumia ASALI YA NYUKI WADOGO:-

1. Inazuia maambukizi kwenye kidonda kwasababu sukari zilizopo kwenye asali zinazuia uwepo wa unyevunyevu na hivyo vijidudu haviwezi kuzaliana

2. Inaua BAKTERIA kwenye kidonda kutokana na uzalishaji wa HYDROGEN PEROXIDE unaofanyika baada ya asali kufanya kitu kinachoitwa "glucose oxidase enzyme reaction"

3. Inasaidia kurudisha ngozi katika hali ya kawaida

4. Inapunguza sana muda wa kidonda kupona

JINSI YA KUFANYA

1. Hakikisha kidonda chako ni kisafi

2. Tafuta gauze ambayo ndio utaifanya kama dressing yako na kisha weka asali kwenye dressing kutokana na ukubwa wa kidonda

3. Weka dressing yenye asali juu ya kidonda chako na kua unabadilisha kila unapoona asali inapungua mana hapo ndio inafanya kazi

Note:
1. kama kidonda chako kinatoa maji sana basi weka asali nyingi zaidi

2. Kama kidonda kimechimbika ndio kitakavyohitaji asali nyingi zaidi na unashauriwa kupaka asali kwenye kitako cha kidonda kwanza kabla hujafunika na dressing

4. Jinsi kidonda kinavyopona ndio idadi ya dressing itakavyopungua.

NOTE:- kama kidonda chako ni kikubwa tunashauri kabla hujaanza kujitibu ni vizuri ukapata ushauri wa daktari wako pia akupe maelezo sahihi zaidi kutokana na ukubwa wa kidonda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni