Jumatano, 18 Mei 2016

MATATIZO YA UZAZI

TATIZO LA UZAZI

Mwanamke kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makuu mawili:

ni hali iitwayo primary infertility,
Ambapo mwanamke hana historia ya kupata uja uzito.

ni hali iitwayo secondary infertility, hapa mwanamke anayo historia  kama alishawahi kupata ujauzito,haijalishi kama alishazaa au alitoa au iliharibika.

Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita infertility au ugumba.

Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.

🌼Maambukizi katika vyanzo vya uzazi,

🌼Hali duni ya lishe na magonjwa sugu,
Pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.

Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanake:

Vyanzo vya matatizo haya zinahusisha aina zote mbili za ugumba primary na secondary,

🌼Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai
"Ovulatory" tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa, ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai, hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa  homoni mwilini,
Tatizo zinaweza likatokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na Dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi.
Tutakuja kuona In shaa Allah.

Dalili za upevushaji wa mayai ziko njingi saana miongoni mwazo ni:

Mwanamke kupata ute wa uzazi ambao uko wa aina tatu:

Pia upevushaji unaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu,ambavyo  unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kushika mimba.

🌼Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija,

Mirija inaweza kuziba, kutanuka,kuweka usaha, au maji,maambukizi katika mirija, au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.

🌼utoaji wa mimba, maambukizi ya Mara kwa Mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija.

Matatizo ya mirija  husababisha ugumba kwa kiasi  kikubwa, ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.

Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi,ambapo linatoka kwa nje badala ya kuwa ndani,
Hali hii kitaalam inaitwa " Endometriosis"
Hili siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa saana lakini linaathiri Baadhi ya wanawake.

Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo, na huwa makali wakati wa hedhi, na husababisha Damu ya hedhi kutoka kidogokidogo,
Mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.

Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambao humuathiri mwanamke, mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri,anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa,
Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vyema naye akafanyiwa uchunguzi endapo wanatafuta mtoto auWA ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina, inaonekana mume hana tatizo na wala mke hana tatizo, hali hii kitaalam inaitwa Unexplained Infertility. Kwa hiyo ni vyema ukafanyiwa uchunguzi wa kina

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni