Ijumaa, 14 Desemba 2018

Kijicho na sababu zake

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.

SABABU ZA KUPATWA NA UCHAWI,JINI,HASADI NA KIJICHO.

Amesema Allah aliyetukuka.

له معقبا ت من بين يديه ومن خلفه يحفظونه من أمر الله

Kila mtu analo kunda la Malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu(Arraad 11).

Allah mtukufu ametuahidi ulinzi kutokana na mambo mbalimbali,wapo wapatwao na matatizo kama mitihani tu Allah amewakadiria ili kuwapima imani zao na halina kuhoji hilo.

لا يسئل عما يفعل وهم يسأ لون.

Haulizwi (Allah) afanyalo bali hao (waja) ni wenye kuulizwa.(Al -anbiyaai 23)

Wengine hupatwa na mitihani kwa njia ya kuwaonya kutokana na makosa yao ili wamrejee Mola wao.

وما أصابكم من مصيبة فبما كسبت أيديكم.

Na haiwi kwa yanayo kupateni kutokana na majanga ni yale yaliyo tokana na mikono yenu.(Ashuuraa 30).

Tutakuletea sababu miongoni mwa sababu za mja kupatwa na mitihani ya Uchawi,Kijicho,Hasadi na Mashetani wa kijini.

(1)Kujiweka mbali na Allah mtukufu,kwani mwenye kuwa mbali na Mola wake rafiki yake ni shetani na ataishi maisha ya dhiki,na mwenye kuwa karibu na Allah basi huhifadhiwa.

(2)Kufanya sherehe zenye munkari na haramu ndani yake na upuuzi, kama Rusha roho,matarumbeta, vigodoro n.k,kwani shetani hushiriki katika sherehe hizo na huwa rahisi kumpata amtakae kwa kumuingia na kumuwekea uchawi.

(3) Kuogopa sana Uchawi mpaka hofu ya Allah ikamuondoka mtu, ikawa haamini kama Allah anaweza kumuhifadhi na shari za wachawi.

(4) Kutosoma Adhkari za asubuhi na jioni pamoja na kupuuza adhkari za kulalia pamoja na adhkari nyinginezo kama kuingia chooni n.k.

(5)Mwanadamu kumtamani jini kama kumuoa au kuolewa na jini,au jini kumtamani mwanadamu kimapenzi na ikawa mtu huyo hafanyi adhkari yoyote.

(6)Mwanadamu kumuudhi jini kwa kumrushia kitu kama takataka,kummwagia maji ,kumkwaa au kumkanyaga na ikawa mtu huyo hana Adhkari,jini hughadhibika na kumuingia kwa urahisi.

(7) Kulala uchi au na nguo zenye kuonesha umbile la mtu na ikawa amelala bila ya kusoma Adhkari za kulalia.

(8)Kupenda tabia za kishetani kama kuigiza katika Filam mtu yeye ni jini au Zimwi.

(9)Kutembea ufukweni mwa bahari na kuogelea na pia kukaa maeneo hayo na viguo vifupi hali ya kuwa hajasoma adhkari za kinga mtu huyo asubuhi na jioni.

(10)Kukaa chooni muda mrefu iwe kujisaidi au kupenda tu kuchezea maji huko chooni.

(11) Kupenda kuzungumza au kuimba au kulia akiwa chooni.

(12) Kutotajwa Mwenyezi Mungu ndani ya nyumba kwa kutosomwa Qurani au kusikilizwa mawaidha,ikawa ni nyumba ya muziki na  Tamthilia.

(13)Kufaya madhambi makubwa kama Uzinifu,Ulawiti,Ulevi,Wizi,Ushirikina na mengine mfano wa hayo.

(14)Kuhuzunika sana baada ya tukio la simanzi hadi kuchanganyikiwa,kama kufiwa au kufurahi sana kupita kiasi hadi kukufuru kama kuvua nguo mbele za watu,kucheza ngoma na kadhalika.

(15)Kurusha mawe sehemu zilizo hamwa kama magofu,magari mabovu,mapango na miti mikubwa.

Hayo yote endapo yatafanywa na mtu asiyesoma adhkari za kujikiga asubuhi na jioni basi ni rahisi kupatikana na majini,uchawi ,hasadi na kijicho.

Tubadilikeni ndiyo ufumbuzi wa matatizo yetu.

إن الله لا يغير ما بقوم حتى يغير ما بأنفسهم

Hakika Allah habadilishi yaliyo kwa watu mpaka wabadilishe yaliyoko nafsini mwao.(Arraad 11).

Kwa tiba nasaha na ushauri wasiliana nami +255715849684

Jumanne, 13 Novemba 2018

Kushindwa kufanya tendo

بسم الله الرحمن الرحيم.

PONYO NA SULUHISHO LA MARADHI.

Tiba ya mtu aliyefungwa asiweze kuliendea tendo la ndoa.

Ipo namna ya uchawi ambayo lengo ni kuwatenganisha wanandoa,au kumfanya mwanaume asioe au mwanamke asioleke,si jingine ni kifungo cha kumzuia kufanya tendo la ndoa.

Dalili kwa mwanaume.

1,Kushindwa kumuingilia mkewe kwa kupoteza nguvu karibu ya tendo hilo,
2,Kutotokua na nguvu za kiume zenye kutosheleza mpaka kuhofia kuoa.
3,Kuishiwa nguvu ghafla katikati ya tendo la ndoa.
4,Mwanaume kumchukia mkewe bila ya sababu na kutomtamani hata kama nguvu zipo.

Dalili kwa mwanamke.

1,Kuchukia tendo la ndoa na kutohisi raha.
2,Kukosa ute na maumivu makali pamoja na michubuko.
3,Kukosa hedhi kabisa au kupata hedhi chache.
4,Maumivu makali sana ya tumbo siku za hedhi hasa chini ya kitovu.
5,Kutoshika mimba kabisa au kutoka mimba mara kwa mara.
5,Kuzaa kwa tabu kupita kiasi au kulazimu upasuaji mara kwa mara.
6,Kutohisi kabisa uchungu wa uzazi hata kama siku zimetimia na kupitiliza.
7,Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa au kabla.
8,Kutembea kitu tumboni au mwilini wote

Dawa yake.

1,Mizizi saba ya mti uitwao Mwamba mji (Ausajal Ahmara).
2,Ubani Dhukhra vijiko vitatu vya chakula.
3,Maji lita sita.

Maandalizi.

Vioshe kwanza kisha changanya vitu hivyo halafu chemsha  mpaka maji yafikie lita tano,baada ya hapo acha ipoe  kisha somea aya za Ruqya rudia mara tatu.

Matumizi.

Anywe muathirika wa uchawi kikombe cha chai kidogo kila baada ya masaa  manne usiku na mchana mpaka dawa iishe ila mja mzito na mtoto mdogo wasitumie dawa hii.

Faida ya dawa.

Dawa hii inabatilisha vifungo vya namna nyingi vya uchawi na imewanufaisha wengi.

Tanbihi.

Dawa hii itunzwe kwa kuwekwa ndani ya Friji,au ipashwe moto kila siku asubuhi na jioni ili isiharibike.

Matokeo ya dawa.

Siyo ajabu mgonjwa akaharisha kidogo,au kukojoa sana,au mwanamke kupata hedhi nyingi kidogo,hali zote hizo ni namna ya kusafisha,pia siyo ajabu akahisi kumtembea vitu mwilini au kufunguka mafundo, hiyo ni dalili ya kuwa na jini ,akiona hivyo basi asomewe Ruqya ya kisheria atapona lnshaallah.
+255715849684

Alhamisi, 4 Oktoba 2018

Lengo la mashetan

بسم الله الرحمن الحيم.

NINI LENGO LA MASHETANI KUMUAMRISHA MJA KUFANYA IBADA?

Utawasikia wanasema.

Alhamdulillaahi Mashetani yake yanampeleka kwenye kheri.

(a)Wamemuamrisha kuswali mpaka sasa hivi anaswali.

(b) Akizini wanapanda na kukemea hawataki uchafu na tena ataumwa.

(c) Hawataki atembee kichwa wazi bila ya kujifunika, sasa hivi ushungi na mtu.

(d) Wanamlinda kila wakimwendea wachawi anapandisha na kuwakimbiza.

(e) Hawataki anywe pombe akinywa anaumwa kwelikweli.

(f) Asikubali kuolewa hao ndiyo watakao mchagulia mume bora.

(g) Watamfundisha uganga ili asaidie watu maana jamii inateseka kwa maradhi na shida mbalimbali.

(h) Kuamrisha kilinge kifungwe mwezi wa Ramadhani kwa sababu ni mwezi mtukufu haifai kucheza ngoma, ni mwezi wa toba .

(i) Akiolewa ni lazima ashikwe sikio tujulishwe, akipata mimba tujulishwe, akizaa tujulishwe, ili tumlinde na ubaya wa mahasidi.

Maneno hayo ukiyatazama ni mazuri, lakini lengo ni baya kwa mwenye kuyakubali.

Aliwahi kusema Aliy bnu Abiy Twaalibi Allah amridhie.

.كلمـــــــة حق أريد بهــــــا باطل.

Maneno ya kweli lakini lengo ni batili.

lkiwa Allah na Mtume wake wamekuamrisha kufanya mema na kuacha mabaya huku wakikuonya endapo utapuuza basi utaadhibiwa, na Allah ni mkali wa kuadhibu kuliko yeyote yule.

Yawaje Allah umpuuze halafu ufanye utiifu kwa kumuogopa  Shetani ambae hana uwezo wa kukuadhibu kumshinda Allah mtukufu?, huo ni ujinga.

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ.

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi (Alkawthar - 2).

Ina maana yote hayo uliyo mkabidhi Shetani huamini kwamba Mola wako anaweza kuyasimamia?, Au wewe ni katika wale alio wataja Allah katika aya hii tukufu?.

اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّهِ ۚ أُولَٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ.

Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi la Shetani ndilo lenye kupata khasara (Mujaadilah 19).

Kama ulikua hujui leo jua kwamba Allah ndiye mlinzi pekee kwako, hao Mashetani unao wategemea ni kujidanganya tu na kujipeleka Jahannamu.

اللَّهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُمْ مِنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ.

Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu(Albaqarah - 257).

Hivi mpaka leo hujaelewa na kuzingatia mafundisho haya ya Mtume wako swalla llaahu alayhi wasallama pindi alipokua akimfundisha Swahaba wake lbnu Abbaasi Allah amridhie yeye na baba yake?.

إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللَّهِ وَاعْلَمْ أَنَّ الْأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ لَكَ وَلَوْ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إِلَّا بِشَيْءٍٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ.ُ(رواه الترمذي عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ).

Ukitaka kuomba muombe Allah, na  ukitaka msaada taka msaada kwa Allah, Tambua hakika watu lau walijikusanya ili kukunufaisha, hawato kunufaisha ila kwa lile alilo kuandikia Allah, Na lau watu wakijikusanya ili kukudhuru hawato kudhuru ila lile alilo kuandikia Allah (Ameipokea Tirmidh kutokana na lbnu Abbaas).

Huo uganga hautokosa kupiga Ramli na kuwapa wagonjwa masharti yaambatanayo na Shirki kama kumchinjia jini n.k.

  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ
  ،من أتى عرافاً فسأله عن شيء فصدقه لم تقبل له صلاة أربعين يوما ( ، رواه مسلم)

Amesema Mtume swalla llaahu alayhi wasallama, Mwenye kumuendea  mpiga Ramli akamuuliza jambo na akamsadiki basi haikubaliwi swala kwake siku arobaini ( Muslimu).

  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ : مَنْ أَتَى عَرَّافًا أَوْ كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ فِيمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ (رواه الحاكم).

Amesema Mtume swalla llaahu alayhi waalihi wasallama, Mwenye kumwendea Mpiga ramli au Kuhani na akamsadikisha katika ayasemayo, Hakika amekufuru kilicho teremka kwa Muhamadi (Alhaakimu)

Shetani ni Shetani hawezi kuwa mwema hata siku moja atabaki kuwa adui, hizo ni ghiliba za kuwafanya watu wajinga  wamtii kwa sababu ya maslahi madogo ya duniani  ili aende nao motoni.

إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ

Hakika Shet'ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni (Alfaatwir-6).

kama una Mashetani wa tabia hiyo usijidhanie umepata bado huo ni upotevu,  kasomewe Ruqya uondokane na  ibada za kuwatii Mashetani.

Sisi kazi yetu ni kubainisha, mwenye kuongoa ni Allah pekee.big
.0715849684

Jumamosi, 17 Machi 2018

Wanawake muhim

Aina 10 ya Wanawake wanaopendwa na wanaume

WENYE MSIMAMO 
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio. 

WAPENDA USAWA 
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50. 

WANAOJUA MAPENZI 
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani. 

MARAFIKI 
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani. 

WA WAZI 
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo. 

WANAOJITEGEMEA  
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja. 

WASIO NA PRESHA 
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi. 

MARIDADI  
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano. 

WANAORIDHIKA 
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke. 

WA MMOJA 
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.

Jumatano, 17 Januari 2018

Swala ya maiti

Most of us Don't know what we are saying during Salat Al-janaaza ( Burial prayers):

JINSI YA KUMSWALIA MAITI JIFUNZE HAPO CHINI

1- After the First Takbeer : Recite Surat Al-Fatiha.
Ukisha nuia na kusema Allah akbaru Soma suratil Alfatiha (Alhamdu)

2-After the Second Takbeer: Salat Al-Ibrahimiyya ( Allahumma Salli Alaa Muhammad Wa Alaa Aali Muhammad....to the end ).
Imam akisema Allahu Akbaru unamfuatisha na kumsalia mtume
Allahumma Salli Alaa Muhammad Wa Alaa Aali Muhammad..mpaka mwisho

3-Ater the Third Takbeer: Pray for the dead but according how its narrated from our Prophet S.A.W. One of them is:( Allahummagfir lahuu warhamhu wathabbit-hu Alal qawlu Athaabit ).

Imam akisema tena Allah akabaru  unamuombea maiti dua...kwa kusema hivi...( Allahummagfir lahuu warhamhu wathabbit-hu Alal qawlu Athaabit )

4- Then lastly after the Fourth Takbeer: Say: ( Allahumma laa tuharrimnaa ajrahuu wa laa taftinna ba'adahuu )
And you should pray for all Muslims.
Imam akisha sema Allahu akabru  unaomba tena :dua kw akusema
( Allahumma laa tuharrimnaa ajrahuu wa laa taftinna ba'adahuu )

5- And lastly end the prayer with one Salaam to the right ( Just once ).
Imam akitoa Salam na wewe unatoa salam umemaliza kumswalia maitı.

Please share if you think its right for the benefit of others.
May Allah S.W forgive us our sins.

TAFADHALI WAPELEKEE NA WENZAKO WAPATE KUJIFUNZA KUMSWALIA MAITI