Ijumaa, 14 Desemba 2018
Kijicho na sababu zake
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.
SABABU ZA KUPATWA NA UCHAWI,JINI,HASADI NA KIJICHO.
Amesema Allah aliyetukuka.
له معقبا ت من بين يديه ومن خلفه يحفظونه من أمر الله
Kila mtu analo kunda la Malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu(Arraad 11).
Allah mtukufu ametuahidi ulinzi kutokana na mambo mbalimbali,wapo wapatwao na matatizo kama mitihani tu Allah amewakadiria ili kuwapima imani zao na halina kuhoji hilo.
لا يسئل عما يفعل وهم يسأ لون.
Haulizwi (Allah) afanyalo bali hao (waja) ni wenye kuulizwa.(Al -anbiyaai 23)
Wengine hupatwa na mitihani kwa njia ya kuwaonya kutokana na makosa yao ili wamrejee Mola wao.
وما أصابكم من مصيبة فبما كسبت أيديكم.
Na haiwi kwa yanayo kupateni kutokana na majanga ni yale yaliyo tokana na mikono yenu.(Ashuuraa 30).
Tutakuletea sababu miongoni mwa sababu za mja kupatwa na mitihani ya Uchawi,Kijicho,Hasadi na Mashetani wa kijini.
(1)Kujiweka mbali na Allah mtukufu,kwani mwenye kuwa mbali na Mola wake rafiki yake ni shetani na ataishi maisha ya dhiki,na mwenye kuwa karibu na Allah basi huhifadhiwa.
(2)Kufanya sherehe zenye munkari na haramu ndani yake na upuuzi, kama Rusha roho,matarumbeta, vigodoro n.k,kwani shetani hushiriki katika sherehe hizo na huwa rahisi kumpata amtakae kwa kumuingia na kumuwekea uchawi.
(3) Kuogopa sana Uchawi mpaka hofu ya Allah ikamuondoka mtu, ikawa haamini kama Allah anaweza kumuhifadhi na shari za wachawi.
(4) Kutosoma Adhkari za asubuhi na jioni pamoja na kupuuza adhkari za kulalia pamoja na adhkari nyinginezo kama kuingia chooni n.k.
(5)Mwanadamu kumtamani jini kama kumuoa au kuolewa na jini,au jini kumtamani mwanadamu kimapenzi na ikawa mtu huyo hafanyi adhkari yoyote.
(6)Mwanadamu kumuudhi jini kwa kumrushia kitu kama takataka,kummwagia maji ,kumkwaa au kumkanyaga na ikawa mtu huyo hana Adhkari,jini hughadhibika na kumuingia kwa urahisi.
(7) Kulala uchi au na nguo zenye kuonesha umbile la mtu na ikawa amelala bila ya kusoma Adhkari za kulalia.
(8)Kupenda tabia za kishetani kama kuigiza katika Filam mtu yeye ni jini au Zimwi.
(9)Kutembea ufukweni mwa bahari na kuogelea na pia kukaa maeneo hayo na viguo vifupi hali ya kuwa hajasoma adhkari za kinga mtu huyo asubuhi na jioni.
(10)Kukaa chooni muda mrefu iwe kujisaidi au kupenda tu kuchezea maji huko chooni.
(11) Kupenda kuzungumza au kuimba au kulia akiwa chooni.
(12) Kutotajwa Mwenyezi Mungu ndani ya nyumba kwa kutosomwa Qurani au kusikilizwa mawaidha,ikawa ni nyumba ya muziki na Tamthilia.
(13)Kufaya madhambi makubwa kama Uzinifu,Ulawiti,Ulevi,Wizi,Ushirikina na mengine mfano wa hayo.
(14)Kuhuzunika sana baada ya tukio la simanzi hadi kuchanganyikiwa,kama kufiwa au kufurahi sana kupita kiasi hadi kukufuru kama kuvua nguo mbele za watu,kucheza ngoma na kadhalika.
(15)Kurusha mawe sehemu zilizo hamwa kama magofu,magari mabovu,mapango na miti mikubwa.
Hayo yote endapo yatafanywa na mtu asiyesoma adhkari za kujikiga asubuhi na jioni basi ni rahisi kupatikana na majini,uchawi ,hasadi na kijicho.
Tubadilikeni ndiyo ufumbuzi wa matatizo yetu.
إن الله لا يغير ما بقوم حتى يغير ما بأنفسهم
Hakika Allah habadilishi yaliyo kwa watu mpaka wabadilishe yaliyoko nafsini mwao.(Arraad 11).
Kwa tiba nasaha na ushauri wasiliana nami +255715849684
Jumanne, 13 Novemba 2018
Kushindwa kufanya tendo
بسم الله الرحمن الرحيم.
PONYO NA SULUHISHO LA MARADHI.
Tiba ya mtu aliyefungwa asiweze kuliendea tendo la ndoa.
Ipo namna ya uchawi ambayo lengo ni kuwatenganisha wanandoa,au kumfanya mwanaume asioe au mwanamke asioleke,si jingine ni kifungo cha kumzuia kufanya tendo la ndoa.
Dalili kwa mwanaume.
1,Kushindwa kumuingilia mkewe kwa kupoteza nguvu karibu ya tendo hilo,
2,Kutotokua na nguvu za kiume zenye kutosheleza mpaka kuhofia kuoa.
3,Kuishiwa nguvu ghafla katikati ya tendo la ndoa.
4,Mwanaume kumchukia mkewe bila ya sababu na kutomtamani hata kama nguvu zipo.
Dalili kwa mwanamke.
1,Kuchukia tendo la ndoa na kutohisi raha.
2,Kukosa ute na maumivu makali pamoja na michubuko.
3,Kukosa hedhi kabisa au kupata hedhi chache.
4,Maumivu makali sana ya tumbo siku za hedhi hasa chini ya kitovu.
5,Kutoshika mimba kabisa au kutoka mimba mara kwa mara.
5,Kuzaa kwa tabu kupita kiasi au kulazimu upasuaji mara kwa mara.
6,Kutohisi kabisa uchungu wa uzazi hata kama siku zimetimia na kupitiliza.
7,Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa au kabla.
8,Kutembea kitu tumboni au mwilini wote
Dawa yake.
1,Mizizi saba ya mti uitwao Mwamba mji (Ausajal Ahmara).
2,Ubani Dhukhra vijiko vitatu vya chakula.
3,Maji lita sita.
Maandalizi.
Vioshe kwanza kisha changanya vitu hivyo halafu chemsha mpaka maji yafikie lita tano,baada ya hapo acha ipoe kisha somea aya za Ruqya rudia mara tatu.
Matumizi.
Anywe muathirika wa uchawi kikombe cha chai kidogo kila baada ya masaa manne usiku na mchana mpaka dawa iishe ila mja mzito na mtoto mdogo wasitumie dawa hii.
Faida ya dawa.
Dawa hii inabatilisha vifungo vya namna nyingi vya uchawi na imewanufaisha wengi.
Tanbihi.
Dawa hii itunzwe kwa kuwekwa ndani ya Friji,au ipashwe moto kila siku asubuhi na jioni ili isiharibike.
Matokeo ya dawa.
Siyo ajabu mgonjwa akaharisha kidogo,au kukojoa sana,au mwanamke kupata hedhi nyingi kidogo,hali zote hizo ni namna ya kusafisha,pia siyo ajabu akahisi kumtembea vitu mwilini au kufunguka mafundo, hiyo ni dalili ya kuwa na jini ,akiona hivyo basi asomewe Ruqya ya kisheria atapona lnshaallah.
+255715849684
Alhamisi, 4 Oktoba 2018
Lengo la mashetan
بسم الله الرحمن الحيم.
NINI LENGO LA MASHETANI KUMUAMRISHA MJA KUFANYA IBADA?
Utawasikia wanasema.
Alhamdulillaahi Mashetani yake yanampeleka kwenye kheri.
(a)Wamemuamrisha kuswali mpaka sasa hivi anaswali.
(b) Akizini wanapanda na kukemea hawataki uchafu na tena ataumwa.
(c) Hawataki atembee kichwa wazi bila ya kujifunika, sasa hivi ushungi na mtu.
(d) Wanamlinda kila wakimwendea wachawi anapandisha na kuwakimbiza.
(e) Hawataki anywe pombe akinywa anaumwa kwelikweli.
(f) Asikubali kuolewa hao ndiyo watakao mchagulia mume bora.
(g) Watamfundisha uganga ili asaidie watu maana jamii inateseka kwa maradhi na shida mbalimbali.
(h) Kuamrisha kilinge kifungwe mwezi wa Ramadhani kwa sababu ni mwezi mtukufu haifai kucheza ngoma, ni mwezi wa toba .
(i) Akiolewa ni lazima ashikwe sikio tujulishwe, akipata mimba tujulishwe, akizaa tujulishwe, ili tumlinde na ubaya wa mahasidi.
Maneno hayo ukiyatazama ni mazuri, lakini lengo ni baya kwa mwenye kuyakubali.
Aliwahi kusema Aliy bnu Abiy Twaalibi Allah amridhie.
.كلمـــــــة حق أريد بهــــــا باطل.
Maneno ya kweli lakini lengo ni batili.
lkiwa Allah na Mtume wake wamekuamrisha kufanya mema na kuacha mabaya huku wakikuonya endapo utapuuza basi utaadhibiwa, na Allah ni mkali wa kuadhibu kuliko yeyote yule.
Yawaje Allah umpuuze halafu ufanye utiifu kwa kumuogopa Shetani ambae hana uwezo wa kukuadhibu kumshinda Allah mtukufu?, huo ni ujinga.
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ.
Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi (Alkawthar - 2).
Ina maana yote hayo uliyo mkabidhi Shetani huamini kwamba Mola wako anaweza kuyasimamia?, Au wewe ni katika wale alio wataja Allah katika aya hii tukufu?.
اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّهِ ۚ أُولَٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ.
Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi la Shetani ndilo lenye kupata khasara (Mujaadilah 19).
Kama ulikua hujui leo jua kwamba Allah ndiye mlinzi pekee kwako, hao Mashetani unao wategemea ni kujidanganya tu na kujipeleka Jahannamu.
اللَّهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُمْ مِنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ.
Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu(Albaqarah - 257).
Hivi mpaka leo hujaelewa na kuzingatia mafundisho haya ya Mtume wako swalla llaahu alayhi wasallama pindi alipokua akimfundisha Swahaba wake lbnu Abbaasi Allah amridhie yeye na baba yake?.
إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلْ اللَّهَ وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللَّهِ وَاعْلَمْ أَنَّ الْأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ لَكَ وَلَوْ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إِلَّا بِشَيْءٍٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ.ُ(رواه الترمذي عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ).
Ukitaka kuomba muombe Allah, na ukitaka msaada taka msaada kwa Allah, Tambua hakika watu lau walijikusanya ili kukunufaisha, hawato kunufaisha ila kwa lile alilo kuandikia Allah, Na lau watu wakijikusanya ili kukudhuru hawato kudhuru ila lile alilo kuandikia Allah (Ameipokea Tirmidh kutokana na lbnu Abbaas).
Huo uganga hautokosa kupiga Ramli na kuwapa wagonjwa masharti yaambatanayo na Shirki kama kumchinjia jini n.k.
قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ
،من أتى عرافاً فسأله عن شيء فصدقه لم تقبل له صلاة أربعين يوما ( ، رواه مسلم)
Amesema Mtume swalla llaahu alayhi wasallama, Mwenye kumuendea mpiga Ramli akamuuliza jambo na akamsadiki basi haikubaliwi swala kwake siku arobaini ( Muslimu).
قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ : مَنْ أَتَى عَرَّافًا أَوْ كَاهِنًا فَصَدَّقَهُ فِيمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ (رواه الحاكم).
Amesema Mtume swalla llaahu alayhi waalihi wasallama, Mwenye kumwendea Mpiga ramli au Kuhani na akamsadikisha katika ayasemayo, Hakika amekufuru kilicho teremka kwa Muhamadi (Alhaakimu)
Shetani ni Shetani hawezi kuwa mwema hata siku moja atabaki kuwa adui, hizo ni ghiliba za kuwafanya watu wajinga wamtii kwa sababu ya maslahi madogo ya duniani ili aende nao motoni.
إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ
Hakika Shet'ani ni adui yenu, basi mfanyeni kuwa ni adui. Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Motoni (Alfaatwir-6).
kama una Mashetani wa tabia hiyo usijidhanie umepata bado huo ni upotevu, kasomewe Ruqya uondokane na ibada za kuwatii Mashetani.
Sisi kazi yetu ni kubainisha, mwenye kuongoa ni Allah pekee.big
.0715849684
Jumanne, 17 Aprili 2018
Jumamosi, 17 Machi 2018
Wanawake muhim
Aina 10 ya Wanawake wanaopendwa na wanaume
WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.
WANAORIDHIKA
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
Jumatano, 17 Januari 2018
Swala ya maiti
Most of us Don't know what we are saying during Salat Al-janaaza ( Burial prayers):
JINSI YA KUMSWALIA MAITI JIFUNZE HAPO CHINI
1- After the First Takbeer : Recite Surat Al-Fatiha.
Ukisha nuia na kusema Allah akbaru Soma suratil Alfatiha (Alhamdu)
2-After the Second Takbeer: Salat Al-Ibrahimiyya ( Allahumma Salli Alaa Muhammad Wa Alaa Aali Muhammad....to the end ).
Imam akisema Allahu Akbaru unamfuatisha na kumsalia mtume
Allahumma Salli Alaa Muhammad Wa Alaa Aali Muhammad..mpaka mwisho
3-Ater the Third Takbeer: Pray for the dead but according how its narrated from our Prophet S.A.W. One of them is:( Allahummagfir lahuu warhamhu wathabbit-hu Alal qawlu Athaabit ).
Imam akisema tena Allah akabaru unamuombea maiti dua...kwa kusema hivi...( Allahummagfir lahuu warhamhu wathabbit-hu Alal qawlu Athaabit )
4- Then lastly after the Fourth Takbeer: Say: ( Allahumma laa tuharrimnaa ajrahuu wa laa taftinna ba'adahuu )
And you should pray for all Muslims.
Imam akisha sema Allahu akabru unaomba tena :dua kw akusema
( Allahumma laa tuharrimnaa ajrahuu wa laa taftinna ba'adahuu )
5- And lastly end the prayer with one Salaam to the right ( Just once ).
Imam akitoa Salam na wewe unatoa salam umemaliza kumswalia maitı.
Please share if you think its right for the benefit of others.
May Allah S.W forgive us our sins.
TAFADHALI WAPELEKEE NA WENZAKO WAPATE KUJIFUNZA KUMSWALIA MAITI
Jumapili, 19 Novemba 2017
Umuhim wa Mtindi
💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞FAIDA YA MAZIWA MTINDI KWA MWANAMKE💞💞💞💞.
MAZIWA MTINDI YANA SIRI KUBWA KWA WANAWAKE NI WENGI HAWAYAPENDI ILA MTOTO WA KIKE JITAHIDI USIKOSE KUNYWA GLASS MOJA YA MAZIWA HAYA KILA SIKU
💕💕💕💕💕
➡ HAYA HUSAIDIANA NA BAKTERIA WA UKENI KATIKA KULINDA UKE KUZUIA ATHARI ZA FUNGUS KWA KUNYWA NA KUPAKA UKENI
💕💕💕
➡PIA UKIYATUMIA HUSAIDIA KURUDISHA UMBO LA UKE,HATA KAMA IMETANUKA UTARUDI KAMA ZAMANI TUMIA KWA KUNYWA
💕💕💕
➡HUONDOA HARUFU MBAYA Kukeni UkITUMIA NA KUIPA HARUFU NZURI YA KUVUTIA NA
KUNOGA KWELI HASA UNAPOKUWA UKIFANYA MAPENZI👌
💕💕💕
➡PIA HUFANYA UKE UWE MNATO WAKATI WA KUFANYA MAPENZI
💕💕💕💕💕
JITAHIDI ASUBUHI UKIAMKA KUNYWA MAJI YA MOTO GLASS MBILI,KAA MASAA MAWILI KUNYWA MTINDI PAKITI MOJA NDOGO AU GLASS MOJA KILA SIKU NDANI YA MIEZI SITA HALAFU LETE MLEJESHO HAPA👇PIA KAMA ULIKUWA MHANGA WA FUNGUS UTASHANGAA NATURALLY ZAONDOKA NA KUJIHISI MTAAMU PIA HUONDOA SHOMBO HUKO HARUFU MBAYA
Jumapili, 5 Novemba 2017
Alhamisi, 19 Oktoba 2017
Mfaham mshirikina
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.
*ALAMA ZA KUMJUA MGANGA (MSHIRIKINA) MCHAWI.*
Amesema Allah mtukufu.
ۖ إِنَّهُ مَن يُشرِك بِاللَّهِ فَقَد حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيهِ الجَنَّةَ وَمَأواهُ النّارُ ۖ وَما لِلظّالِمينَ مِن أَنصارٍ.
Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru (Almaaidah 72).
*Zifuatazo ni alama zinazo julisha mganga mshirikina.*
(a) Ni kuuliza jina la mgonjwa au mama yake au baba yake ili imsaidie kujua maradhi ya mgonjwa na kumtibu.
(b) Kutaka athari kwa mgonjwa kama nguo yake au nywele au kucha na kadhakika.
(c) Kumpa mgonjwa hirizi yenye mchoro na maandishi ya herufi za mkato au karatasi yenye maandishi hayo na kumtaka atie ndani ya maji kisha anywe.
(d) Kusoma visomo visivyo sikika au lugha inayo tumika haieleweki.
(e) Kumtaka mgonjwa alete mnyama au ndege mwenye sifa maalumu na kumchinja bila ya kumtaja Allah, *(Bismillaahi)*
(f) Kumpa mgonjwa makaratasi ili ayachome moto au achimbie ardhini au atundike juu.
(g) Kumpa sharti mgonjwa asiguse maji kwa muda maalumu.
(h) Kumwambia mgonjwa jina lake na jina la mzazi wake na kumtajia kilicho mleta kwake mtu huyo.
(i) Kuwa matamshi yake ni kutaka msaada kwa Majini kama kuita *Yaa Sybiyaan wamakataan* na kadhalika.
(j) Kumtenga mgonjwa na watu kwa muda maalumu kwa kukaa chumbani tena kwenye kiza chumbaa kisicho pitisha hata mionzi ya jua.
*Ametukataza Mtume swalla llaahu alayhi wasallama kuwaendea waganga wenye sifa za ushirikina*.
أن النبي صلى الله عليه وسلم قال "من أتى كاهنا أو عرافا فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد صلى الله عليه وسلم" (رواه أحمد.)
Hakika Mtume swalla llaahu alayhi wasallama amesema, Mwenye kumuendea Kuhani au mpiga Ramli na akamsadikisha ayasemayo, hakika amekufuru kile kilicho teremshiwa kwa Muhammadi swalla llaahu alayhi wasallama (Ameipokea Ahmadi).
ٌقالَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلمَ:"مَنْ أتى عَرَّافًا فَسَأَلهُ عَنْ شَئٍ لم تقْبَل لَهُ صَلاةُ أربعينَ ليلة(رواه مسلم).
Amesema Mjumbe wa Allah swalla llaahu alayhi wasallama, Mwenye kumuendea mpiga Ramli, kisha akamuuliza jambo, hatokukubaliwa Swala siku arobaini (Ameipkea Muslimu).
*Akili za kuambiwa changanya na zako,*
*Allah atuhifadhi na mitihani ya washirikina.*
*آمين*.
Jumatano, 18 Oktoba 2017
Kubemenda
Kubemenda Mtoto
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.
Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.
Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!
kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.
Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.
Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.
Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.
Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?
Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;
Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).
Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.
Jumanne, 10 Oktoba 2017
Mshirikina
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.
*ALAMA ZA KUMJUA MGANGA (MSHIRIKINA) MCHAWI.*
Amesema Allah mtukufu.
ۖ إِنَّهُ مَن يُشرِك بِاللَّهِ فَقَد حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيهِ الجَنَّةَ وَمَأواهُ النّارُ ۖ وَما لِلظّالِمينَ مِن أَنصارٍ.
Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru (Almaaidah 72).
*Zifuatazo ni alama zinazo julisha mganga mshirikina.*
(a) Ni kuuliza jina la mgonjwa au mama yake au baba yake ili imsaidie kujua maradhi ya mgonjwa na kumtibu.
(b) Kutaka athari kwa mgonjwa kama nguo yake au nywele au kucha na kadhakika.
(c) Kumpa mgonjwa hirizi yenye mchoro na maandishi ya herufi za mkato au karatasi yenye maandishi hayo na kumtaka atie ndani ya maji kisha anywe.
(d) Kusoma visomo visivyo sikika au lugha inayo tumika haieleweki.
(e) Kumtaka mgonjwa alete mnyama au ndege mwenye sifa maalumu na kumchinja bila ya kumtaja Allah, *(Bismillaahi)*
(f) Kumpa mgonjwa makaratasi ili ayachome moto au achimbie ardhini au atundike juu.
(g) Kumpa sharti mgonjwa asiguse maji kwa muda maalumu.
(h) Kumwambia mgonjwa jina lake na jina la mzazi wake na kumtajia kilicho mleta kwake mtu huyo.
(i) Kuwa matamshi yake ni kutaka msaada kwa Majini kama kuita *Yaa Sybiyaan wamakataan* na kadhalika.
(j) Kumtenga mgonjwa na watu kwa muda maalumu kwa kukaa chumbani tena kwenye kiza chumbaa kisicho pitisha hata mionzi ya jua.
*Ametukataza Mtume swalla llaahu alayhi wasallama kuwaendea waganga wenye sifa za ushirikina*.
أن النبي صلى الله عليه وسلم قال "من أتى كاهنا أو عرافا فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد صلى الله عليه وسلم" (رواه أحمد.)
Hakika Mtume swalla llaahu alayhi wasallama amesema, Mwenye kumuendea Kuhani au mpiga Ramli na akamsadikisha ayasemayo, hakika amekufuru kile kilicho teremshiwa kwa Muhammadi swalla llaahu alayhi wasallama (Ameipokea Ahmadi).
ٌقالَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلمَ:"مَنْ أتى عَرَّافًا فَسَأَلهُ عَنْ شَئٍ لم تقْبَل لَهُ صَلاةُ أربعينَ ليلة(رواه مسلم).
Amesema Mjumbe wa Allah swalla llaahu alayhi wasallama, Mwenye kumuendea mpiga Ramli, kisha akamuuliza jambo, hatokukubaliwa Swala siku arobaini (Ameipkea Muslimu).
*Akili za kuambiwa changanya na zako,*
*Allah atuhifadhi na mitihani ya washirikina.*
*آمين*.
Jumatatu, 9 Oktoba 2017
Mafuta ya nazi
Faida 10 za kutumia Mafuta ya Nazi
1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo:
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula:
Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.
3. Mafuta ya nazi hung’arisha ngozi:
Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha. Pia unaruhusiwa kuyatumia mafuta haya wakati wa masaji.
4. Huongeza nguvu mwilini:
Mafuta ya nazi ni chanzo kizuri cha nguvu ya mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo sifa hii huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’ ambacho ni chakula cha ubongo. Kwahiyo ikiwa unatafuta lift ya kuinua nguvu yako basi chukua kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya nazi weka kwenye kikombe chako cha juisi au uji na utaona maajabu.
5. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya:
Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya. Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!
6. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama:
Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula. Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki kuwa magumu hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.
7. Huzuia maradhi mengi hatari mwilini:
Kama ilivyo katika kuipunguza kolesteroli, mafuta ya nazi yanao uwezo mkubwa katika kuzuia na kutibu magonjwa mengine sababu ya kuwa na kiasi kingi cha asidi iitwayo lauric acid. Utafiti mwingi umeendelea kuthibitisha kuwa hii lauric asidi hubadilishwa kuwa asidi mafuta nyingine ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘monolaurin’ ambayo inayo sifa ya kudhibit na kuvizuia baadhi ya virusi ikiwemo vile vya ukimwi kuziingia na kuzidhuru seli za mwili na kusababisha maradhi mwilini. Ili kutibu virusi vya ukimwi inashauriwa kunywa glasi 4 za tui la nazi kila siku kwa muda wa miezi mitatu mine na utaona maajabu.
8. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu:
Hii inaweza ikakushangaza kidogo unapoisikia kwa mara ya kwanza lakini tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli na shughuli za ubongo na katika kufanya hivyo kutasaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
9. Hutumika kulainisha uke mkavu:
Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu, kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake tena bila madhara yeyote hasi.
10. Husaidia katika ugonjwa wa mzio/aleji:
Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza, moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
MHIMU: Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani ile ya asili. Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.
Alhamisi, 19 Mei 2016
Hisia
VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA HARAKA KWA Mwanamke
Ni kweli kwamba kuna wanawake wengine huwa hata wakichezewa au kushikwashikwa kila mahali na mwanaume ili apate ashki ya kufanya tendo la ndoa huwa ni kazi bure kwani hamu haimjii haraka au haimjii kabisa na hata akiamua kufanya anafanya tuu ili kumridhisha mwenzake.
Japokuwa hisia za mwanamke zipo mbali mno lakini kama mwanaume atamshikashika pande tofautitofauti za mwili wake na kumletea utundu wa hapa na pale basi hisia huja na akajiskia ni mwenye kuhitaji tendo hilo la kiutu uzima na akaweza ipasavyo.
Kama na wewe ni mmojawapo kati ya wahanga wa tatizo hilo nakushauri tumia dawa hizi zenye kupatikana kiurahisi kabisa katika mazingira yetu kwani ni zenye kusaidia kutibu kabisa matatizo ya kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake kwa haraka zaidi.
MBEGU ZA FENESI
Mbegu za fenesi zinafahamika na kila mmoja,ni zile ambazo zinapatikana ndani ya tunda la fenesi,kama mwanamke anapendelea kula tunda hizo kuanzia kumi au zaidi kila baada ya siku 4 baada ya kuzichemsha na kuiva vizuri basi hamu ya kufanya tendo la ndoa zitamzidia na atakuwa ni mwenye kutamani kufanya mchezo huo kwa matamanio makubwa sana....hii ni tiba nzuri kwa wanawake wenye tatizo hili.
UJI WA ULEZI
Wanawake wanashauriwa kunywa uji wa ulezi kila siku asubuhi kwani uji huu una uwezo wa kuamsha hisia za mapenzi
MUHOGO MBICHI
Imethibitishwa kwamaba kama muhogo mbichi kama utapendelewa kuliwa na mwanamke kiasi cha vipande5 pia vina uwezo wa kuamsha hisia za mapenzi au tendo la ndoa kwa wanawake.
KOROSHO
Nazo zinatajwa ni nzuri sana kwa kumuongezea mwanamke hamu ya kufanya tendo la ndoa akiwa ni mwenye kuzila mara kwa mara
Swaumu
FAIDA ZA FUNGA
MTUME MUHHAMADI rehema na amani ziwe juu yake amesema :: FUNGENI MPATE AFYA
pindi unapo kula chakula mfumo wa mmengenyo wa chakula huvunja vunja CARBOHYDRATE kuwa katika GLUCOSE(sukari) kwa ajili ya kuupa nguvu mwili hivyo glucose hufyonzwa kutoka katika njia za mmengenyo na kupelekwa katika damu kisha huenda mpaka kwenye cell na kuzalisha nguvu na kujenga mwili
sasa usipo kula mwili hupungukiwa na glucose katika damu na hapo huanza kutafuta stoo (store) ya mwili inayo itwa GLYCOGEN na gylcogen inapo ishiwa basi huchoma mafuta na misuli iliyo ongezeka ili kuupa mwili nguvu.
kwa hiyo kutokana na hayo maelezo hapo juu utajua zaid faida ya kufunga kama ifaatavyo
© tibazakissuna.blogspot.com
1) HUTIBU MARADHI YA MOYO
Kama tulivyoona kua mafuta mwilin hutumika kwa wingi pindi unapo kua umefunga hivyo kwa muda wa masiku 29 mpaka 30 utakua na selli zenye mafuta CHACHE na kufanya moyo kufanya kazi ipasavyo
2) HUPUNGUZA UZITO
Kwa watu walio wanene na wenye vitambi hii ina maana kua GLYCOGEN (stoo ya chakula katika mwili ) ni kubwa hivyo unapo funga glycogen zenu zitatumika ipasavyo na kufanya mwili kupungua
3) HUTIBU KISUKARI TYPE 2
katika ugonjwa huu selli za mwilim hua sio sikivu kwa insulini (kidhibiti cha glucose katika damu) hivyo mtu akifunga insulini hua na nguvu (sensitive) ya kutuma signal kuiambia GLUCOSE KISAFIRISHI kusafirisha glucose katika seli kwani ugonjwa huu hutokea pale SIGNAL hiyo inapo zuiwa na kusababisha selli kuto chukua sukari hiyo hivyo hulepelekea sukar kuwa juu
4) HUTIBU KIHARUSI NA MISTUKO
Unapo funga mfumo wako wa moyo na mishipa (cardiovascular) hufanya kazi vyema na kutibia magonjwa yalio katika mfumo huo sasa kama tunavyojua kama mfumo wako wa damu utafanya kazi vyema inamaana uwezo wa ubongo kupata oxygen ya kutosha utakuepo hivyo ubongo utafanya kazi ipasavyo
5) HUPUMZISHA MMENGENYO
Maradhi mengi hukulia na kukomaa katika mfumo wa mmengenyo na kisha husambaa kwenye damu pindi mmengenyo unapo kua umepumzika hali ya vijidudu vinavyo leta maradhi hufaa na mwili kujisafisha kupitia metabolism
6) HUONGEZA UMRI
ni kweli kua kula bila kushibisha tumbo hukuongezea umri wa afya njema katika maisha hivyo ubora wa kufunga ni mara mbili yake
7) HUKUZA UWEZO WA UBONGO (akili)
kufunga imethibitishwa kuongeza uwezo wa ubongo kwani husaidia kuzalishwa kwa protein inayoitwa ( brain-derived neurotrophic factor (BDNF.)} kutoka 50 mpaka 400 ambayo husaidia kulinda ubongo kutokana na mabadiliko na pia kuzalisha neurons
© tibazakissuna.blogspot.com
8) HUTIBU NGOZI NA CHUNUSI
kwakua mwili unapata pumziko la kusaga na kusambaza chakula basi huamishia nguvu zake katika kujenga mwili na kuuboresha haswa kuanzia kwenye ngozi
9) HUKUTIBUA ASTHMA NA MATATIZO YA USINGIZI
funga huweza kuonda tatizo hili kwa kupunguza chumvi na maji mwilini na pia hupunguza uvimbe wa tissue hali inayo weza msaidia mtu kulala vyema na kuondosha shida ya kupumua
10) HUTIBU NAFSI
#TABIA huanza kama uamuzi kisha hua Tabia ambapo hukua na kua mraibu/teja (addicted) na utajua kua upo addicted pindi unapo taka kuliacha jambo hilo na kushindwa hapo jua upo katika hali ya addiction
Allah mjuzi zaidi ila ili kuibadilisha tabia ya mtu huchukua masiku 30
hivyo REHAB ( sehemu za kurekebisha tabia ) hua ni siku 30 na WAISLAM tunafunga siku 29 mpaka 30
hivyo miongoni mwetu tuna ingia kufunga ili kutibu maradhi yaliyo ingia katika nafsi mfano
KUVUTA SIGARA BANGI NA UNYWAJI POMBE
KUJICHUA > njia hii hua ni njia bora zaid ya kujikinga kwani mfumo wa divide and conquer huingia vyema katika swala la funga na kukusaidia kumiliki matamanio yako na kujihifadhi
UZINIFU > mwenzi huu ni mwenz wa kujihifadhi kwanzia macho mpaka utendaji na ukifunga matamanio hupungua kwa kiasi kikubwa wanasayansi wamethibitisha hili kua njia nyepes na yenye kusaidia bila madhara
KUSENGENYA NA KUTUKANA > mwenzi huu hukupa haya na aibu ya kufikiria mara mbili jambo kabla hujaliendea jambo hivyo hukufunza aibu ukiwa na AIBU UNAKUA NA ADABU
HIVYO KUA MKWELI KWA SWAUMU YAKO ISHIKE NAFSI YAKO NA UTAPONA KWA UWEZO WA ALLAH MARADHI YA NAFSI NDANI YA MASIKU 29 MPAKA 30
© mketo.blogspot.com
Jumatano, 18 Mei 2016
Jitibu vidonda
KUTIBU VIDONDA KWA KUTUMIA ASALI
ASALI ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu vidonda na ambayo imekua ikitumika kwa miaka mingi sana. Historia inaonyesha hata wakati wa vita zamani wanajeshi walikua wanatumia Asali kutibu vidonda!!
Kwanini Asali inatibu vidonda???
Asali ina tabia na faida zifuatazo ambazo zinasaidia uponyeshaji hasa hasa ukitumia ASALI YA NYUKI WADOGO:-
1. Inazuia maambukizi kwenye kidonda kwasababu sukari zilizopo kwenye asali zinazuia uwepo wa unyevunyevu na hivyo vijidudu haviwezi kuzaliana
2. Inaua BAKTERIA kwenye kidonda kutokana na uzalishaji wa HYDROGEN PEROXIDE unaofanyika baada ya asali kufanya kitu kinachoitwa "glucose oxidase enzyme reaction"
3. Inasaidia kurudisha ngozi katika hali ya kawaida
4. Inapunguza sana muda wa kidonda kupona
JINSI YA KUFANYA
1. Hakikisha kidonda chako ni kisafi
2. Tafuta gauze ambayo ndio utaifanya kama dressing yako na kisha weka asali kwenye dressing kutokana na ukubwa wa kidonda
3. Weka dressing yenye asali juu ya kidonda chako na kua unabadilisha kila unapoona asali inapungua mana hapo ndio inafanya kazi
Note:
1. kama kidonda chako kinatoa maji sana basi weka asali nyingi zaidi
2. Kama kidonda kimechimbika ndio kitakavyohitaji asali nyingi zaidi na unashauriwa kupaka asali kwenye kitako cha kidonda kwanza kabla hujafunika na dressing
4. Jinsi kidonda kinavyopona ndio idadi ya dressing itakavyopungua.
NOTE:- kama kidonda chako ni kikubwa tunashauri kabla hujaanza kujitibu ni vizuri ukapata ushauri wa daktari wako pia akupe maelezo sahihi zaidi kutokana na ukubwa wa kidonda
Uzito
KUPUNGUZA UZITO, MAFUTA MWILINI, TUMBO
Unaweza kupunguza uzito wako, mafuta mwilini, tumbo ukiwa nyumbani kwako popote ulipo kwa kutumia ASALI na MDALASINI WA UNGA
Swali ni je, kwanini ASALI na MDALASINI??!
a) ASALI na MDALASINI kwa pamoja zinaongeza spidi ya mfumo wa umeng'enyaji chakula
b) Pia ASALI na MDALASINI zinazuia mwili kutunza MAFUTA mabaya
c) MDALASINI unachochea umeng'enyaji wa SUKARI YA MWILINI( BLOOD SUGAR) vizuri zaidi na hivyo kuzia uzalishaji wa mafuta( fatty acids or fat)
Fata steps zifuatazo kutengeneza mchanganyiko huo:-
1. Chemsha maji kikombe kimoja cha chai na changanya kijiko kimoja cha chai cha MDALASINI WA UNGA
2. Funika mchanganyiko wako kwa dakika 20-30 ili upoe vizuri( usichanganye asali wakati maji ya moto sana unaweza kuua ENZYMES zilizopo kwenye asali)
3. Chuja vipande pande vya mdalasini au unaweza kuviacha kama unaweza kuvinywa na kisha changanya kijiko kimoja cha chai au cha chakula cha ASALI kwenye maji yaliyopoa na kinywaji chako kinakua tayari.
4. Kunywa mchanganyiko huu kila siku ASUBUHI NA MAPEMA angalau NUSU SAA( DAKIKA 30) kabla hujanywa chai.
Kunywa mchanganyiko huu kwa wiki kadhaa kuweza kuona tofauti.
NOTE: pamoja na kunywa mchanganyiko huu ni vizuri pia kubadilisha mfumo wa maisha kwa kufanya mazoezi kidogo, kunywa maji mengi, kupunguza vyakula vya mafuta na sukari nyingi.
Tunawaomba KUSHARE kwa wingi ili kuwajuza watu wengi na pia usiache KULIKE PAGE yetu kupata dondoo nyingi zaidi za asali.
[18/04 05:01] Big mketo: MATUMIZI YA ASALI KWA AFYA YA NGOZI YAKO
Unaweza tumia ASALI kuondokana na matatizo mengi ya ngozi kama vile MAFUTA MENGI,CHUNUSI nk. Lakini pia kuipa muonekano mzuri zaidi ngozi yako!!
Tumia ASALI ukiwa umekaa nyumbani kwako na huku ukiendelea kufanya shughuli nyingine.
ASALI ina faida zifuatazo kwenye ngozi:-
1. Inasaidia kunyonya UNYEVU(MOISTURE) wa ziada kwenye ngozi yako na kuzuia maambukizi ya ngozi
2. Asali ina tabia za kiantibakteria ambazo zinasaidia kuponyesha chunusi na pia kuzuia kujirudia.
3. Asali ina virutubisho vingi ambavyo vinaipa ngozi afya lakini pia inazuia ngozi kuzeeka
4. Asali inafungua matundu(PORES) ya ngozi na kufanya iwe rahisi kwe ngozi kutoa uchafu
Pamoja na faida nyingine nyingi ambazo wale wanaotumia tungependa watuambie pia kwa kucomment jinsi wanavyoitumia ASALI
MATATIZO YA UZAZI
TATIZO LA UZAZI
Mwanamke kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makuu mawili:
ni hali iitwayo primary infertility,
Ambapo mwanamke hana historia ya kupata uja uzito.
ni hali iitwayo secondary infertility, hapa mwanamke anayo historia kama alishawahi kupata ujauzito,haijalishi kama alishazaa au alitoa au iliharibika.
Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita infertility au ugumba.
Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.
🌼Maambukizi katika vyanzo vya uzazi,
🌼Hali duni ya lishe na magonjwa sugu,
Pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.
Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanake:
Vyanzo vya matatizo haya zinahusisha aina zote mbili za ugumba primary na secondary,
🌼Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai
"Ovulatory" tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa, ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai, hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini,
Tatizo zinaweza likatokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na Dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi.
Tutakuja kuona In shaa Allah.
Dalili za upevushaji wa mayai ziko njingi saana miongoni mwazo ni:
Mwanamke kupata ute wa uzazi ambao uko wa aina tatu:
Pia upevushaji unaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu,ambavyo unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kushika mimba.
🌼Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija,
Mirija inaweza kuziba, kutanuka,kuweka usaha, au maji,maambukizi katika mirija, au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.
🌼utoaji wa mimba, maambukizi ya Mara kwa Mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija.
Matatizo ya mirija husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa, ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.
Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi,ambapo linatoka kwa nje badala ya kuwa ndani,
Hali hii kitaalam inaitwa " Endometriosis"
Hili siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa saana lakini linaathiri Baadhi ya wanawake.
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo, na huwa makali wakati wa hedhi, na husababisha Damu ya hedhi kutoka kidogokidogo,
Mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.
Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambao humuathiri mwanamke, mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri,anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa,
Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vyema naye akafanyiwa uchunguzi endapo wanatafuta mtoto auWA ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina, inaonekana mume hana tatizo na wala mke hana tatizo, hali hii kitaalam inaitwa Unexplained Infertility. Kwa hiyo ni vyema ukafanyiwa uchunguzi wa kina
Jumapili, 21 Februari 2016
Mashetani
SHETANI NA MARADHI
USINGIZI
ZIPO DALILI NYINGI KABISA ZA MASHETANI AMBAZO MTU AKIWA NA HIZO . BASI AJUE ANA MAGONJWA AMBAYO YANAMGUSO WA MASHETANI NA ZIPO ALAMA (4) AMBAZO ZINABAINISHA AINA ZA MARADHI AMBAZO SHETANI HUMPA MTU.
KUGUSWA SEHEMU
MARANYINGI ANAYEGUSWA NA MASHETANI SEHEMU MAALUMU HUKUSUDIWA APATWE NA MARADHI YA ENEO MOJA KAMA MGUU, MKONO ,ULIMI, SEHEMU ZA SIRI, MGUSO HUU HUSABABISHA MAUMIVU AU KUPOOZA AU KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA KILE KIUNGO,HUSIKA AU KUSHINDWA KUFANYA TENDO LA NDOA KUTOKANA NA MAUMIVU MAKALI, AU HATA KUPASUKA, AU KUTOKUHISI LADHA AU ULIMI KUVIMBA NA KUSHINDWA KUONGEA.
KUGUSWA MZIMA
AINA HII YA MGUSO HUMSABABISHIA ALIYEGUSWA AWE NA MKAKAMO WA MISHIPA , AU DEGEDEGE AU MAUMIVU MAKALI YA VIUNGO , MTU ALIYEPATA ATHARI HII HUISI MWILI MZIMA UMEKAZA NA HAWEZI LOLOTE
KUGUSWA MZUNGUKO
HUU HUWA KAMA UPEPO ISIPOKUWA UNA MADHARA YA KUWA KAMA UMEFUNIKWA NA KITU NA UKAZIBWA PUMZI ,AU UKAPALIWA NA KITU LAKINI AINA HII NI AGHRABU SANA KUCHUKUA MUDA MREFU . KABLA HIYO HALI HAIJAONDOKA
, INGAWA NI MGUSO WA MUDA MFUPI LAKINI UNA MAUMIVU MAKALI SANA KWA KUWA KUZIBWA PUMZI SI JAMBO DOGO.
KUGUSWA KWA DAIMA.
YEYOTE AMBAYE SHETANI AMEMGUSA KWA DAIMA AIDHA KWA KUTUMIKA KICHAWI AU KIKAWAIDA , HUWA NA MARADHI YA KUENDELEA AMBAYO HUMPELEKEA MPAKA KUFANYIWA TIBA ZA KISHIRIKINA KAMA KUCHORWA KUPAKWA DAWA HALI HANA NGUO N.K JAMBO LA MSINGI NI KUANGALIA KWA MAKINI NINI UFANYE.
NIMEONELEA NIANDIKE HAYO ILI UJIULIZE KUWA MARADHI YAKO YAPO YA AINA IPI KAMA HUTOJALI NITAFUTE ILI TUANGALIE TIBA AMBAYO ITAKUSAIDIA INSHAALLAH.
ZIPO DALILI AMBAZO HUMPATA MTU USINGIZI NA HIZI NI DALILI MUHIMU AMBAZO ZINATOFAUTIANA NA ZA USINGIZI WA KAWAIDA . LAKINI HIZI ZOTE NINAZOZITAJA HAPA NI ZILE ZA MASHETANI NA KICHAWI AMBAZO HUMPATA MTU .
KUKOSA USINGIZI:
MTU ANAPOPANDA KITANDANI HUKOSA USINGIZI MPAKA UPITE MUDA MREFU NDIPO HUUPATA , MTU HUYU HUANDAMWA NA MARADHI YA KICHWA MARA KWA MARA KWA KUKOSA USINGIZI.
HAMANIKO:
KUKOSA RAHA USINGIZINI , KUSHTUKA NA KUHEMA MARA KWA MARA AU KIFUA KUBANA USINGIZINI
KUTAFUNA MENO:
KUNA WALE AMBAO PINDI WANAPOKUWA USINGIZINI HUTAFUNA MENO HIZO NI DALILI ZA MASHETANI.
KUFUKUZWA NA WANYAMA ,AU KUWAONA , MBWA, PAKA ,CHUI, NGAMIA, PANYA ,MBWEA, TANDU.USINGIZINI HIZI NAZO NI DALILI ZA KUWA UNASHETANI
NDOTO ZA KUTISHA:
HII NAYO NI MIONGONI MWA DALILI ZA MASHETANI KUOTA NDOTO MBAYA ZA KUTISHA AMBAZO ZINAMFANYA MPAKA AOGOPE KULALA. NI MIONGONI MWA DALILI KUU
KUFANYA TENDO LA NDOA , KUOLEWA, KUZAA ,KUNYONYESHA:
YEYOTE AMBAYE ANAOTA VITU HIVI BILA SHAKA HUYO ANASUMBULIWA NA MASHETANI MAHABA AMBAYO WENGI HUISHIA KUVISHWA PETE AU KUCHINJIWA WANYAMA N.K . TAMBUA KUWA HAWA MASHETANI HUWA WANASUMBUA SANA SANA , LAKINI INSHAALLAH NITAFUTE UFANYIWE TIBA SAHIHI NAWE UFURAHIE NDOA YAKO.
KUZUNGUMZA USINGIZINI . KUTEMBEA, KULIA, KUCHEKA.
KAMA UNAFANYA HIVI USINGIZINI NI MIONGONI MWA DALILI ZA MASHETANI . AMBAO NI LAZIMA UFANYE JITIHADA YAONDOKE.
KUOTA MAKABURINI , WATU WALIOKUFA, KUANGUKA, KUPAA.
NDUGU YANGU TAMBUA YA KWAMBA , MPANGO WA MUNGU SI MASHETANI YAKAE MWILINI MWETU. KAMA UNAMATATIZO YA MAJINI MAHABA , KUUMWA NA MENO , AU FANGASI wasiliana nae upate tiba