Alhamisi, 19 Oktoba 2017

Mfaham mshirikina

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته.

*ALAMA ZA KUMJUA MGANGA  (MSHIRIKINA) MCHAWI.*

Amesema Allah mtukufu.

ۖ إِنَّهُ مَن يُشرِك بِاللَّهِ فَقَد حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيهِ الجَنَّةَ وَمَأواهُ النّارُ ۖ وَما لِلظّالِمينَ مِن أَنصارٍ.

Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru (Almaaidah 72).

*Zifuatazo ni alama zinazo julisha mganga mshirikina.*

(a) Ni kuuliza jina la mgonjwa au mama yake au baba yake ili imsaidie kujua maradhi ya mgonjwa na kumtibu.

(b) Kutaka athari kwa mgonjwa kama nguo yake au nywele au kucha na kadhakika.

(c) Kumpa mgonjwa hirizi yenye mchoro na maandishi ya herufi za mkato  au karatasi yenye maandishi hayo na kumtaka atie ndani ya maji kisha anywe.

(d) Kusoma visomo visivyo sikika au lugha inayo tumika haieleweki.

(e) Kumtaka mgonjwa alete mnyama au ndege mwenye sifa maalumu na kumchinja bila ya kumtaja Allah, *(Bismillaahi)*

(f) Kumpa mgonjwa makaratasi ili ayachome moto au achimbie ardhini au atundike juu.

(g) Kumpa sharti mgonjwa asiguse maji kwa muda maalumu.

(h) Kumwambia mgonjwa jina lake na jina la mzazi wake na kumtajia kilicho mleta kwake mtu huyo.

(i) Kuwa matamshi yake ni kutaka msaada kwa Majini kama kuita *Yaa Sybiyaan wamakataan* na kadhalika.

(j) Kumtenga mgonjwa na watu kwa muda maalumu kwa kukaa chumbani tena kwenye kiza chumbaa kisicho pitisha hata mionzi ya jua.

*Ametukataza Mtume swalla llaahu alayhi wasallama kuwaendea waganga wenye sifa za ushirikina*.

أن النبي صلى الله عليه وسلم قال "من أتى كاهنا أو عرافا فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد صلى الله عليه وسلم" (رواه أحمد.)

Hakika Mtume swalla llaahu alayhi wasallama amesema, Mwenye kumuendea Kuhani au mpiga Ramli na akamsadikisha ayasemayo, hakika amekufuru kile kilicho teremshiwa kwa  Muhammadi swalla llaahu alayhi wasallama (Ameipokea Ahmadi).

ٌقالَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلمَ:"مَنْ أتى عَرَّافًا فَسَأَلهُ عَنْ شَئٍ لم تقْبَل لَهُ صَلاةُ أربعينَ ليلة(رواه مسلم).

Amesema Mjumbe wa Allah swalla llaahu alayhi wasallama, Mwenye kumuendea mpiga Ramli, kisha akamuuliza jambo, hatokukubaliwa Swala siku arobaini (Ameipkea Muslimu).

*Akili za kuambiwa changanya na zako,*

*Allah atuhifadhi na mitihani ya washirikina.*

*آمين*.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni