Alhamisi, 19 Mei 2016

Hisia

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA HARAKA KWA Mwanamke

Ni kweli kwamba kuna wanawake wengine huwa hata wakichezewa au kushikwashikwa kila mahali na mwanaume ili apate ashki ya kufanya tendo la ndoa huwa ni kazi bure kwani hamu haimjii haraka au haimjii kabisa na hata akiamua kufanya anafanya tuu ili kumridhisha mwenzake.

Japokuwa hisia za mwanamke zipo mbali mno lakini kama mwanaume atamshikashika pande tofautitofauti za mwili wake na kumletea utundu wa hapa na pale basi hisia huja na akajiskia ni mwenye kuhitaji tendo hilo la kiutu uzima na akaweza ipasavyo.

Kama na wewe ni mmojawapo kati ya wahanga wa tatizo hilo nakushauri tumia dawa hizi zenye kupatikana kiurahisi kabisa katika mazingira yetu kwani ni zenye kusaidia kutibu kabisa matatizo ya kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake kwa haraka zaidi.

  MBEGU ZA FENESI
Mbegu za fenesi zinafahamika na kila mmoja,ni zile ambazo zinapatikana ndani ya tunda la fenesi,kama mwanamke anapendelea kula tunda hizo kuanzia kumi au zaidi kila baada ya siku 4 baada ya kuzichemsha na kuiva vizuri basi hamu ya kufanya tendo la ndoa zitamzidia na atakuwa ni mwenye kutamani kufanya mchezo huo kwa matamanio makubwa sana....hii ni tiba nzuri kwa wanawake wenye tatizo hili.

              
UJI WA ULEZI
Wanawake wanashauriwa kunywa uji wa ulezi kila siku asubuhi kwani uji huu una uwezo wa kuamsha hisia za mapenzi

                     
                   
   MUHOGO MBICHI
Imethibitishwa kwamaba kama muhogo mbichi kama utapendelewa kuliwa na mwanamke kiasi cha vipande5 pia vina uwezo wa kuamsha hisia za mapenzi au tendo la ndoa kwa wanawake.

  KOROSHO
Nazo zinatajwa ni nzuri sana kwa kumuongezea mwanamke hamu ya kufanya tendo la ndoa akiwa ni mwenye kuzila mara kwa mara

Swaumu

FAIDA ZA FUNGA

MTUME MUHHAMADI  rehema na amani ziwe juu yake amesema :: FUNGENI MPATE AFYA

pindi unapo kula chakula mfumo wa mmengenyo wa chakula huvunja vunja CARBOHYDRATE  kuwa katika GLUCOSE(sukari) kwa ajili ya kuupa nguvu mwili hivyo glucose hufyonzwa kutoka katika njia za mmengenyo na kupelekwa katika damu kisha huenda mpaka kwenye cell na kuzalisha nguvu na kujenga mwili

sasa usipo kula mwili hupungukiwa na glucose katika damu na hapo huanza kutafuta stoo (store) ya mwili inayo itwa GLYCOGEN na gylcogen inapo ishiwa basi huchoma mafuta na misuli iliyo ongezeka ili kuupa mwili nguvu.
  kwa hiyo kutokana na hayo maelezo hapo juu utajua zaid faida ya kufunga kama ifaatavyo

© tibazakissuna.blogspot.com

1) HUTIBU MARADHI YA MOYO

Kama tulivyoona kua mafuta mwilin hutumika kwa wingi pindi unapo kua umefunga hivyo kwa muda wa masiku 29 mpaka 30 utakua na selli zenye mafuta CHACHE na kufanya moyo kufanya kazi ipasavyo

2) HUPUNGUZA UZITO

Kwa watu walio wanene na wenye vitambi hii ina maana kua GLYCOGEN (stoo ya chakula katika  mwili ) ni kubwa hivyo unapo funga glycogen zenu zitatumika ipasavyo na kufanya mwili kupungua

3) HUTIBU KISUKARI TYPE 2

katika ugonjwa huu selli za mwilim hua sio sikivu kwa insulini (kidhibiti cha glucose katika damu)  hivyo mtu akifunga insulini hua na nguvu (sensitive) ya kutuma signal  kuiambia GLUCOSE KISAFIRISHI kusafirisha glucose katika seli  kwani ugonjwa huu hutokea pale SIGNAL hiyo inapo zuiwa na kusababisha selli kuto chukua sukari hiyo hivyo hulepelekea sukar kuwa juu

4) HUTIBU KIHARUSI NA MISTUKO

Unapo funga mfumo wako wa moyo na mishipa (cardiovascular) hufanya kazi vyema na kutibia magonjwa yalio katika mfumo huo sasa kama tunavyojua kama  mfumo wako wa damu utafanya kazi vyema inamaana uwezo wa ubongo kupata oxygen ya kutosha utakuepo hivyo ubongo utafanya kazi ipasavyo

5) HUPUMZISHA MMENGENYO

Maradhi mengi hukulia na kukomaa katika mfumo wa mmengenyo na kisha husambaa kwenye damu pindi mmengenyo unapo kua umepumzika hali ya vijidudu vinavyo leta maradhi hufaa na mwili kujisafisha kupitia metabolism

6) HUONGEZA UMRI

ni kweli kua kula bila kushibisha tumbo hukuongezea umri wa afya njema katika maisha hivyo ubora wa kufunga ni mara mbili yake

7) HUKUZA UWEZO WA UBONGO (akili)

kufunga imethibitishwa kuongeza uwezo wa ubongo kwani husaidia kuzalishwa kwa protein inayoitwa ( brain-derived neurotrophic factor (BDNF.)} kutoka 50 mpaka 400 ambayo husaidia kulinda ubongo kutokana na mabadiliko na pia kuzalisha neurons

© tibazakissuna.blogspot.com

8) HUTIBU NGOZI NA CHUNUSI

kwakua mwili unapata pumziko la kusaga na kusambaza chakula basi huamishia nguvu zake katika kujenga mwili na kuuboresha haswa kuanzia kwenye ngozi

9) HUKUTIBUA ASTHMA NA MATATIZO YA USINGIZI

funga huweza kuonda tatizo hili kwa kupunguza chumvi na maji mwilini na pia hupunguza uvimbe wa tissue hali inayo weza msaidia mtu kulala vyema na kuondosha shida ya kupumua

10) HUTIBU NAFSI

#TABIA huanza kama uamuzi kisha hua Tabia ambapo hukua na kua mraibu/teja (addicted)  na utajua kua upo addicted pindi unapo taka kuliacha jambo hilo na kushindwa hapo jua upo katika hali ya addiction
Allah mjuzi zaidi ila ili kuibadilisha tabia ya mtu huchukua masiku 30

hivyo REHAB ( sehemu za kurekebisha tabia ) hua ni siku 30 na WAISLAM tunafunga siku 29 mpaka 30
hivyo miongoni mwetu tuna ingia kufunga ili kutibu maradhi yaliyo ingia katika nafsi mfano

KUVUTA SIGARA BANGI NA UNYWAJI POMBE

KUJICHUA > njia hii hua ni njia bora zaid ya kujikinga kwani mfumo wa divide and conquer huingia vyema katika swala la funga na kukusaidia kumiliki matamanio yako na kujihifadhi

UZINIFU >  mwenzi huu ni mwenz wa kujihifadhi kwanzia macho mpaka utendaji na ukifunga matamanio hupungua kwa kiasi kikubwa wanasayansi wamethibitisha hili kua njia nyepes na yenye kusaidia bila madhara

KUSENGENYA NA KUTUKANA > mwenzi huu hukupa haya na aibu ya kufikiria mara mbili jambo kabla hujaliendea jambo hivyo hukufunza aibu ukiwa na AIBU UNAKUA NA ADABU

HIVYO KUA MKWELI KWA SWAUMU YAKO ISHIKE NAFSI YAKO NA UTAPONA KWA UWEZO WA ALLAH MARADHI YA NAFSI NDANI YA MASIKU 29 MPAKA 30
© mketo.blogspot.com

Jumatano, 18 Mei 2016

Jitibu vidonda

KUTIBU VIDONDA KWA KUTUMIA ASALI

ASALI ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu vidonda na ambayo imekua ikitumika kwa miaka mingi sana. Historia inaonyesha hata wakati wa vita zamani wanajeshi walikua wanatumia Asali kutibu vidonda!!

Kwanini Asali inatibu vidonda???

Asali ina tabia na faida zifuatazo ambazo zinasaidia uponyeshaji hasa hasa ukitumia ASALI YA NYUKI WADOGO:-

1. Inazuia maambukizi kwenye kidonda kwasababu sukari zilizopo kwenye asali zinazuia uwepo wa unyevunyevu na hivyo vijidudu haviwezi kuzaliana

2. Inaua BAKTERIA kwenye kidonda kutokana na uzalishaji wa HYDROGEN PEROXIDE unaofanyika baada ya asali kufanya kitu kinachoitwa "glucose oxidase enzyme reaction"

3. Inasaidia kurudisha ngozi katika hali ya kawaida

4. Inapunguza sana muda wa kidonda kupona

JINSI YA KUFANYA

1. Hakikisha kidonda chako ni kisafi

2. Tafuta gauze ambayo ndio utaifanya kama dressing yako na kisha weka asali kwenye dressing kutokana na ukubwa wa kidonda

3. Weka dressing yenye asali juu ya kidonda chako na kua unabadilisha kila unapoona asali inapungua mana hapo ndio inafanya kazi

Note:
1. kama kidonda chako kinatoa maji sana basi weka asali nyingi zaidi

2. Kama kidonda kimechimbika ndio kitakavyohitaji asali nyingi zaidi na unashauriwa kupaka asali kwenye kitako cha kidonda kwanza kabla hujafunika na dressing

4. Jinsi kidonda kinavyopona ndio idadi ya dressing itakavyopungua.

NOTE:- kama kidonda chako ni kikubwa tunashauri kabla hujaanza kujitibu ni vizuri ukapata ushauri wa daktari wako pia akupe maelezo sahihi zaidi kutokana na ukubwa wa kidonda

Uzito

KUPUNGUZA UZITO, MAFUTA MWILINI, TUMBO

Unaweza kupunguza uzito wako, mafuta mwilini, tumbo ukiwa nyumbani kwako popote ulipo kwa kutumia ASALI na MDALASINI WA UNGA

Swali ni je, kwanini ASALI na MDALASINI??!

a) ASALI na MDALASINI kwa pamoja zinaongeza spidi ya mfumo wa umeng'enyaji chakula

b) Pia ASALI na MDALASINI zinazuia mwili kutunza MAFUTA mabaya

c) MDALASINI unachochea umeng'enyaji wa SUKARI YA MWILINI( BLOOD SUGAR) vizuri zaidi na hivyo kuzia uzalishaji wa mafuta( fatty acids or fat)

Fata steps zifuatazo kutengeneza mchanganyiko huo:-

1. Chemsha maji kikombe kimoja cha chai na changanya kijiko kimoja cha chai cha MDALASINI WA UNGA

2. Funika mchanganyiko wako kwa dakika 20-30 ili upoe vizuri( usichanganye asali wakati maji ya moto sana unaweza kuua ENZYMES zilizopo kwenye asali)

3. Chuja vipande pande vya mdalasini au unaweza kuviacha kama unaweza kuvinywa na kisha changanya kijiko kimoja cha chai au cha chakula cha ASALI kwenye maji yaliyopoa na kinywaji chako kinakua tayari.

4. Kunywa mchanganyiko huu kila siku ASUBUHI NA MAPEMA angalau NUSU SAA( DAKIKA 30) kabla hujanywa chai.

Kunywa mchanganyiko huu kwa wiki kadhaa kuweza kuona tofauti.

NOTE: pamoja na kunywa mchanganyiko huu ni vizuri pia kubadilisha mfumo wa maisha kwa kufanya mazoezi kidogo, kunywa maji mengi, kupunguza vyakula vya mafuta na sukari nyingi.

Tunawaomba KUSHARE kwa wingi ili kuwajuza watu wengi na pia usiache KULIKE PAGE yetu kupata dondoo nyingi zaidi za asali.
[18/04 05:01] Big mketo: MATUMIZI YA ASALI KWA AFYA YA NGOZI YAKO

Unaweza tumia ASALI kuondokana na matatizo mengi ya ngozi kama vile MAFUTA MENGI,CHUNUSI nk. Lakini pia kuipa muonekano mzuri zaidi ngozi yako!!

Tumia ASALI ukiwa umekaa nyumbani kwako na huku ukiendelea kufanya shughuli nyingine.

ASALI ina faida zifuatazo kwenye ngozi:-

1. Inasaidia kunyonya UNYEVU(MOISTURE) wa ziada kwenye ngozi yako na kuzuia maambukizi ya ngozi

2. Asali ina tabia za kiantibakteria ambazo zinasaidia kuponyesha chunusi na pia kuzuia kujirudia.

3. Asali ina virutubisho vingi ambavyo vinaipa ngozi afya lakini pia inazuia ngozi kuzeeka

4. Asali inafungua matundu(PORES) ya ngozi na kufanya iwe rahisi kwe ngozi kutoa uchafu

Pamoja na faida nyingine nyingi ambazo wale wanaotumia tungependa watuambie pia kwa kucomment jinsi wanavyoitumia ASALI

MATATIZO YA UZAZI

TATIZO LA UZAZI

Mwanamke kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makuu mawili:

ni hali iitwayo primary infertility,
Ambapo mwanamke hana historia ya kupata uja uzito.

ni hali iitwayo secondary infertility, hapa mwanamke anayo historia  kama alishawahi kupata ujauzito,haijalishi kama alishazaa au alitoa au iliharibika.

Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita infertility au ugumba.

Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu.

🌼Maambukizi katika vyanzo vya uzazi,

🌼Hali duni ya lishe na magonjwa sugu,
Pia huathiri hali hii ya ugumba kwa mwanamke.

Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa mwanake:

Vyanzo vya matatizo haya zinahusisha aina zote mbili za ugumba primary na secondary,

🌼Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai
"Ovulatory" tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa, ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai, hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa  homoni mwilini,
Tatizo zinaweza likatokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na Dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi.
Tutakuja kuona In shaa Allah.

Dalili za upevushaji wa mayai ziko njingi saana miongoni mwazo ni:

Mwanamke kupata ute wa uzazi ambao uko wa aina tatu:

Pia upevushaji unaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalumu,ambavyo  unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kushika mimba.

🌼Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija,

Mirija inaweza kuziba, kutanuka,kuweka usaha, au maji,maambukizi katika mirija, au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.

🌼utoaji wa mimba, maambukizi ya Mara kwa Mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija.

Matatizo ya mirija  husababisha ugumba kwa kiasi  kikubwa, ambacho ni kati ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.

Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi,ambapo linatoka kwa nje badala ya kuwa ndani,
Hali hii kitaalam inaitwa " Endometriosis"
Hili siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa saana lakini linaathiri Baadhi ya wanawake.

Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo, na huwa makali wakati wa hedhi, na husababisha Damu ya hedhi kutoka kidogokidogo,
Mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.

Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambao humuathiri mwanamke, mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri,anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa,
Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa hiyo ni vyema naye akafanyiwa uchunguzi endapo wanatafuta mtoto auWA ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina, inaonekana mume hana tatizo na wala mke hana tatizo, hali hii kitaalam inaitwa Unexplained Infertility. Kwa hiyo ni vyema ukafanyiwa uchunguzi wa kina