Jumatano, 18 Mei 2016

Uzito

KUPUNGUZA UZITO, MAFUTA MWILINI, TUMBO

Unaweza kupunguza uzito wako, mafuta mwilini, tumbo ukiwa nyumbani kwako popote ulipo kwa kutumia ASALI na MDALASINI WA UNGA

Swali ni je, kwanini ASALI na MDALASINI??!

a) ASALI na MDALASINI kwa pamoja zinaongeza spidi ya mfumo wa umeng'enyaji chakula

b) Pia ASALI na MDALASINI zinazuia mwili kutunza MAFUTA mabaya

c) MDALASINI unachochea umeng'enyaji wa SUKARI YA MWILINI( BLOOD SUGAR) vizuri zaidi na hivyo kuzia uzalishaji wa mafuta( fatty acids or fat)

Fata steps zifuatazo kutengeneza mchanganyiko huo:-

1. Chemsha maji kikombe kimoja cha chai na changanya kijiko kimoja cha chai cha MDALASINI WA UNGA

2. Funika mchanganyiko wako kwa dakika 20-30 ili upoe vizuri( usichanganye asali wakati maji ya moto sana unaweza kuua ENZYMES zilizopo kwenye asali)

3. Chuja vipande pande vya mdalasini au unaweza kuviacha kama unaweza kuvinywa na kisha changanya kijiko kimoja cha chai au cha chakula cha ASALI kwenye maji yaliyopoa na kinywaji chako kinakua tayari.

4. Kunywa mchanganyiko huu kila siku ASUBUHI NA MAPEMA angalau NUSU SAA( DAKIKA 30) kabla hujanywa chai.

Kunywa mchanganyiko huu kwa wiki kadhaa kuweza kuona tofauti.

NOTE: pamoja na kunywa mchanganyiko huu ni vizuri pia kubadilisha mfumo wa maisha kwa kufanya mazoezi kidogo, kunywa maji mengi, kupunguza vyakula vya mafuta na sukari nyingi.

Tunawaomba KUSHARE kwa wingi ili kuwajuza watu wengi na pia usiache KULIKE PAGE yetu kupata dondoo nyingi zaidi za asali.
[18/04 05:01] Big mketo: MATUMIZI YA ASALI KWA AFYA YA NGOZI YAKO

Unaweza tumia ASALI kuondokana na matatizo mengi ya ngozi kama vile MAFUTA MENGI,CHUNUSI nk. Lakini pia kuipa muonekano mzuri zaidi ngozi yako!!

Tumia ASALI ukiwa umekaa nyumbani kwako na huku ukiendelea kufanya shughuli nyingine.

ASALI ina faida zifuatazo kwenye ngozi:-

1. Inasaidia kunyonya UNYEVU(MOISTURE) wa ziada kwenye ngozi yako na kuzuia maambukizi ya ngozi

2. Asali ina tabia za kiantibakteria ambazo zinasaidia kuponyesha chunusi na pia kuzuia kujirudia.

3. Asali ina virutubisho vingi ambavyo vinaipa ngozi afya lakini pia inazuia ngozi kuzeeka

4. Asali inafungua matundu(PORES) ya ngozi na kufanya iwe rahisi kwe ngozi kutoa uchafu

Pamoja na faida nyingine nyingi ambazo wale wanaotumia tungependa watuambie pia kwa kucomment jinsi wanavyoitumia ASALI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni